HOME

Feb 17, 2012

MAIMARTHA AGOMA MTOTO WAKE KUPIGWA PICHA!!


Aliyewahi kuwa mtangazaji wa kituo cha Televisheni EATV, Maimartha Jesse amesema hivi sasa asingependelea mtoto wake apigwe picha kwa kuhofia mionzi ya kamera.


Maimatha amesema kwamba mtoto wake huyo aliyezaliwa siku za hivi karibuni amebatizwa jina la Francis, amezaliwa katika hospitali ya taifa  Muhimbili Jijini Dar es Salaam, na ni mapema mno kwa watu kumpiga picha hadi siku 40 zipite.


Mai ambaye amefunga ndoa hivi karibuni na mchumba wake anayefahamika kwa jina la Shaa amesema mtoto wake Francis alizaliwa na uzito wa kilo 4 kasoro na hali yake pamoja na mama wa mtoto zinaendelea vizuri.

No comments:

Post a Comment