HOME

Feb 3, 2012

TANZANIA IMEOMBWA KUTAFUTA ADHABU MBADALA KWA WATUHUMIWA!!



















Serikali ya Tanzania imeombwa kutafuta adhabu mbadala kwa ajili ya watuhumiwa wa makosa mbali mbali, wanaotumikia adhabu za vifungo katika magereza nchini.


Jaji mkuu wa Tanzania, mheshimiwa Mohammedi Chande Othman ametoa rai hiyo kwa rais Jakaya Kikwete wakati wa maazimisho ya siku ya sheria nchini, sherehe zilizofanyika kitaifa jijini Dar es Salaam leo.


Kwa mujibu wa jaji mkuu Chande, haja ya kuwepo kwa adhabu mbadala inalenga kukabiliana na wimbi la mrundikano wa mahabusu na wafungwa katika magereza, kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kuchelewa kusikilizwa kwa kesi pamoja na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha.

No comments:

Post a Comment