Tume ya vyuo vikuu nchini Tanzania (TCU) imeanzisha mfumo mpya wa utambuzi, uhakiki na utoaji ithibati ya viwango vya taaluma kwa wanafunzi waliosoma nchi za nje kama sehemu ya kupunguza urasimu.
Katibu mtendaji wa tume hiyo, Profesa Sifuni Mchome amesema kuanzia sasa tume hiyo itatumia mawasiliano ya mtandao wa kompyuta pamoja na kutoa cheti maalumu kitakachoeleza kiwango cha elimu ya mtu husika tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo tume ilikuwa ikiandika barua pekee.
Mbali na kutoa ithibati, tume hiyo pia imeanzisha mfumo wa mawasiliano ya mtandao na taasisi inazoshirikiana nazo, zoezi linaloenda sambamba na uanzishwaji wa mfumo wa kutambua tuzo za vyuo vikuuu, kuwepo kwa vigezo vya ufundishaji pamoja na tathmini ya aina ya walimu wanaofaa kufundisha vyuo vya elimu ya juu nchini.
No comments:
Post a Comment