Feb 20, 2012
BONDIA DERECK CHISORA AACHIWA HURU!!
Bondia Dereck Chisora ameachiwa huru bila ya kufunguliwa jalada la kesi Jijini Munich, baada ya kupigana ngumi kavu kavu na bondia mwenzake wa Uingereza David Haye.
Haye na Chisora walipigana katika mkutano wao na waandishi wa habari, wa kutangaza pambano lao. Polisi bado wanamtafuta Haye ambaye hajulikani alipojificha, kwa ajili ya kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo.
Akizungumzia tukio hilo bondia anayeshikilia mkanda wa WBC, Wladimir Klitschko amesema ugomvi huo umeharibu heshima ya mchezo wa ngumi, na amemtaka Chisora na Haye waadhibiwe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment