HOME

Feb 28, 2012

VETA YAPEWA CHANGAMOTO!!


Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal ameitaka  Mamlaka ya Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA) iwe chanzo cha kuibua ajira kwa kuwaandaa vijana hata walioko mbali kuwa wajasiriamali kwa kutumia mkongo wa mawasiliano.


Dk. Bilal ametoa kauli hiyo kwenye hafla ya kuweka jiwe la msingi chuo cha VETA Makete akiwa katika  ziara yake ya kikazi mkoani Iringa.


AMEsema hivi sasa dunia ipo katika ushindani  na mambo mengi yanakuwa kwa haraka zaidi na hivyo kuwataka waangalie uwezekano wa kutumia mkongo wa mawasiliano katika kukuza elimu ya ufundi kwa walio mbali  na wao wafaidike na elimu hiyo ili waweze kujiajiri.

No comments:

Post a Comment