HOME

Feb 7, 2012

SERIKALI YAONGEZA FEDHA ZA SENSA

Waziri wa fedha Mh. Mustafa Mkulo akizungumza katika semina ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha na Uchumi na Kamati ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii,

Serikali ya Tanzania imelazimika kuongeza Shilingi bilioni 27.1 katika bajeti yake ya sensa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka jana hadi 2015 na hivyo kufanya gharama za kazi hiyo sasa kuwa Shilingi bilioni 141.5 kutoka Shilingi bilioni 114.4.


Akizungumza katika semina ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha na Uchumi na Kamati ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii, Waziri wa Fedha na uchumi Mhe. Mustafa Mkulo amesema gharama za sensa zimeongezeka kutokana na mabadiliko ya bei za bidhaa kama mafuta na gharama nyingine zilizotokea duniani.


Amesema sababu nyingine ya ongezeko hilo ambazo zilibainika baada ya sensa ya majaribio iliyofanyika mwaka jana ni siku za mafunzo kwa wakufunzi na makarani kutotosheleza ikiwa ni pamoja na siku saba zilizopangwa kwa ajili ya kuhesabu watu kuongezwa na kufikia 12.

No comments:

Post a Comment