HOME

Feb 14, 2012

WAUGUZI WATISHIA KUFANYA MGOMO KENYA!!


Wauguzi pamoja na maafisa wa kliniki nchini Kenya wametoa taarifa ya kuanzisha mgomo mpya kufuatia mgogoro wa malipo ya malupulupu yao.


Wameipa serikali wiki tatu za kumaliza mgogoro huo juu ya malipo yao na kupitia chama cha wataalamu wa afya nchini Kenya (KHPS), wamesema wataacha kutoa huduma za afya nchi nzima kushinikiza kulipwa madai yao.


Maafisa hao na wauguzi wamedai kuwa wakati madaktari wakiwa wameongezewa malipo yao kufikia shilingi laki nne za Kenya muuguzi ambaye anashghulika na mgonjwa muda wote amekuwa akilipwa shilingi elfu saba za Kenya.

No comments:

Post a Comment