HOME

Feb 21, 2012

NIKO IMARA KAMA MBUYU - RAIS MUGABE!!


Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amepuuza hofu kuhusu afya yake na kujigamba kuwa yuko imara kama mbuyu huku akiadhimisha umri wa miaka 88 leo.


Akihojiwa na radio inayomilikiwa na serikali jana rais Mugabe amesema iko siku ataugua lakini kwa sasa ni mzima alikaririwa akisema kiongozi huyo ambaye mtawala mwenye umuri mkubwa barani Afrika.


Mugabe ambaye ameliongoza taifa hilo tangu mwaka 1980 nchi hiyo ilipopata uhuru mara kadhaa amekuwa akikanusha kuwa mgonjwa amekuwa akisafiri kwenda nchini Singapore mara kwa mara mwaka huu na msemaji wake akisema kuwa rais alienda kufanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho,huku vyombo vya habari vikiripoti kuwa anasumbuliwa na saratani.

No comments:

Post a Comment