HOME

Feb 9, 2012

WAZIRI MKUU PINDA ANAKUTANA NA MADAKTARI!!


Waziri mkuu mizengo pinda yupo jijini Dar es salaam kutoka Dodoma kushughulikia mgomo wa madaktari ambao umekuwa ukiendelea kwa lengo la kuupatia ufumbuzi.


Hapo jana Mhe. Pinda amekutana na uongozi wa hospitali ya taifa ya muhimbili pamoja  na madaktari bingwa kutoka sekta ya umma na binafsi na wastaafu.


Kuanzia leo saa 3 asubuhi amekuwa katika mkutano na madaktari bingwa, madaktari waliosajiliwa
(registrals) na madaktari walioko kwenye mafunzo kwa vitendo (interns) na wafanyakazi wa hospitali ya  Muhimbili, MOI, Ocean road na wawakilishi kutoka hospitali za mkoa wa
Dar es salaam, kwenye ukumbi wa CPL, Muhimbili.


matarajio ya serikali ni kwamba mazungumzo hayo yataweza kumaliza mgogoro  huu na madaktari wote kurejea kazini na hivyo kurejesha huduma za matibabu katika hali ya kawaida kwa wananchi wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment