HOME

Feb 17, 2012

RAIS WA UJERUMANI AJIUZULU!!


Rais wa Ujerumani Christian Wulff amejiuzulu wadhifa wake baada ya kukabiliwa na kashfa ya kupokea mkopo wa fedha katika njia ambazo si halali, na uungwaji mkono kwake umeshuka sana.


Katika hotuba yake muda mfupi uliopita, Christian Wulff ameshukuru kwa muda aliokaa madarakani kama Rais wa Ujerumani, akaongeza kwamba ofisi hiyo kwa sasa inahitaji mtu mwenye hadhi bora na anayeaminiwa na wananchi ambapo amesema kwa sasa yeye hana hadhi hiyo.


Tangazo lake la kujiuzulu limekuja saa chache baada ya Mwendesha mashtaka mkuu kusema anaazimia kuomba kinga ya Rais Wulff iondolewe ili uchunguzi ufanywe juu ya tuhuma zinazomkabili.

No comments:

Post a Comment