HOME

Feb 23, 2012

SERIKALI YASHINDA KESI YA ''SAMAKI WA MAGUFULI''!!




Mahakama kuu ya Tanzania ,leo imetoa hukumu dhidi ya raia wa tano wa China wanaokabiliwa na kesi ya uvuvi haramu katika ukanda wa Tanzania kwa kutumia meli ya Tawariq 1 maarufu kama ‘Kesi ya Samaki wa Magufuli’.


Hukumu hiyo iliyosomwa na Jaji Agustine Mwarija imeamua washtakiwa wawili kati ya watano ambao ni Hsu Chin Tai, Zhao Hanguing wamekutwa na hatia ya kufanya uvuvi katika ukanda wa bahari ya Hindi na kuhukumiwa faini ya shilingi bilioni moja au kifungo cha miaka 20 jela kwa wote wawili lakini Zhao Hanguing alikutwa na kosa jingine hivyo alitakiwa kulipa faini ya shilingi bilioni 20 au kifungo cha miaka 10 ambapo upande wa mashtaka umeiomba mahakama itaifishe meli waliyokuwa na na jaji akakubali na sasa ni mali ya serikali.


Wengine Hsu Shang Pao, Ca’ Dong Li na Chen Rui Hai wameachiwa huru ambapo Mwarija amesema washtakiwa hao wanaweza kukata rufaa kwani milango iko wazi.


Machi 2009 washtakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kisha kesi hiyo ikahamishiwa Mahakama Kuu wakikabiliwa na makosa ya kuvua samaki bila leseni, kuharibu mazingira katika kina kirefu cha ukanda wa Bahari ya Hindi eneo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment