Spika wa bunge Anna Makinda bungeni. |
Spika wa bunge la Tanzania Mhe. Anna Makinda leo amewaangukia madaktari wanaoendelea kufanya mgomo na kuwasihi kurejea kazini wakati madai yao yakiendelea kushughulikiwa na serikali.
Spika Makinda amesema hayo leo asubuhi wakati akifungua kikao cha bunge ambapo amesema tayari waziri mkuu yupo katika mazungumzo na madaktari na ana matumaini ya kufikia muafaka wa mgogoro huo hii leo kwa kuwa kamati iliyotumwa kushughulikia mgogoro huo ya huduma za jamii imerejea jana usiku na kuwasilisha mapendekezo yake ambapo pia wamezungumza na wakuu wa nchi rais pamoja na waziri mkuu ambao wamekubaliana na mapendekezo hao.
Pia amewasihi wadau mbalimbali,viongozi wa dini kuwasihi madaktari kurejea kazini ili kuoko maisha ya watanzania ambao wanakufa kwa kukosa huduma.
Wakati huo huo taarifa zilizoifikia globu hii hivi punde zinasema katibu mkuu wizara ya afya Bi. Blandina Nyoni na Mganga mkuu Deo Mtasiwa wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi kufuatia mgomo wa madaktari.
No comments:
Post a Comment