Feb 17, 2012
BUKENYA AAGIZWA KUMLIPA MPINZANI WAKE KISIASA!!
Mahakama kuu jijini Kampala nchini Uganda imemwagiza makamu wa rais wa zamani ambaye sasa ni mbunge wa jimbo la Busiro kaskazini Gilbert Bukenya kulipa shilingi milioni 107 za Uganda kwa mpinzani wake kisiasa Hussein Kasta,ambaye ameshinda shauri la uchaguzi.
Agizo hilo limetolewa na msajili na afisa wa mahakama Isaac Muwata Februari 2 mwaka huu wakati alipopokea hukumu ya gharana za kodi.
Bukenya ameagizwa kulipa fedha hizo kwa Bw. Kasta ambaye alidai kulipwa shilingi milioni 606 ambapo hata hivyo shauri hilo liliposikilizwa lilipunguza gharama hadi shilingi milioni 107.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment