HOME

Feb 21, 2012

WATANZANIA KUNUFAIKA NA MADINI!!


Makampuni yanayowekeza katika sekta za nishati na madini nchini Tanzania yametakiwa kuzingatia umuhimu wa kutumia sehemu ya mapato yanayotokana na madini katika kuendeleza jamii za sehemu wanakofanya shughuli za utafutaji madini na nishati.


Waziri wa nishati na madini, William Ngeleja amesema hayo jijini Dar es Salaam leo muda mfupi baada ya kusaini mikataba miwili na kampuni ya Swala Limited ya kutafuta mafuta na gesi katika wlaya za Kilosa na Kilombero mkoani Morogoro na bondfe la Pangani mkoani Tanga.


Kauli ya waziri Ngeleja imefuatia ahadi iliyotolewa na kampuni hiyo ya kugawa bure sehemu ya hisa zake kwa wananchi wazawa wa maeneo husika kama njia ya kuwafanya wanufaike na rasilimali za madini yaliyo katika eneo yao.-

No comments:

Post a Comment