HOME

Feb 7, 2012

CONRAD MURRAY NA JAMES DEBARGE WAFUNGWA JELA MOJA!!


Imebainika kuwa aliyekuwa daktari wa Michael Jackson, Dk Conrad Murray sasa amekutana kifungoni na na aliyekuwa mume wa Janet Jackson, James DeBarge, na kutokana na nafasi zao katika jamii, wawili hawa wamelazimika kukaa karibu ndani ya Jela ya L.A. County.


DeBarge ambaye pia ni mwanamuziki, aliswekwa  jela hiyo ambayo Murray anashikiliwa hivi karibuni kwa kosa la kushambulia na silaha pamoja na kupatikana dawa za kulevya, na yeye pia ametengwa katika sehemu ambayo wafungwa maarufu na wenye kuhitaji ulinzi wa ziada wanawekwa, na hivyo moja kwa moja kujikuta anatumikia kifungo sehemu moja na daktari Murray.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mawanasheria wa DeBarge, mwanamuziki huyu amesema kuwa japo alidumu katika mahusiano ya ndoa na dada wa Michael Jackson kwa kipindi kisinchozidi mwaka,alimchukulia Michaela Jackson kama kaka yake na hivyo anamchukia sana Murray na anajisikia vibaya kukaa karibu naye.   

No comments:

Post a Comment