Mbunge wa vunjo Dk. Augustine Mrema |
Mbunge wa vunjo ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali za mitaa nchini Tanzania, Dkt. Augustine Lyatonga Mrema amesema hatojiuzulu wadhifa wa ubunge kwa kisingizio cha posho ndogo.
Mrema amesema hayo ikiwa ni siku moja baada ya vyombo vya habari kumnukuu spika wa bunge, Bi. Anna Makinda akisema kuwa takribani asilimia sabini ya wabunge wanataka kuacha ubunge kutokana na maslahi madogo wanayopata kama wabunge.
Kwa mujibu wa Bw. Mrema, yeye ameamua kuwatumikia Watanzania pasipo kuweka maslahi yake binafsi na kutolea mfano jinsi alivyothubutu kujiuzulu wadhifa wa uwaziri katikati ya miaka ya tisini kwa kile alichodai kuwa ni kutetea maslahi ya wanyonge.
No comments:
Post a Comment