HOME

Feb 3, 2012

WAAFRIKA WAKASIRISHWA NA UBAGUZI WA RANGI UKRAINE!!


Wakereketwa wa haki za binaadam nchini Ukraine wametoa wito kwa rais wa taifa hilo, Viktor Yanukovych, kutokomeza ubaguzi wa rangi baada ya gazeti moja katika mji wa Ternopil, kuchapisha mchoro ulioonyesha wanafunzi wa kiume wa asili ya Kiarabu na Kiafrika wakimpigania msichana mwenye asili ya Ukraine.


Katika mchoro huo wanafunzi hao wamechorwa kwa mfano wa nyani.


Gazeti hilo lijulikanalo kama Nowa Ternopil Hazeta, limesema kuwa hivyo ndivyo lilivyoamua kuonyesha jinsi mapigano kati ya wanafunzi wenye asili wa Kiafrika na Kiarabu katika klabu moja ya usiku mjini humo wakati wakinywa pombe.


Kwenye ukurasa wa kwanza kulikuwa na kichwa cha habari kisemacho "damu ya Waafrika na Waarabu ilimwagika wakipigania malaya wetu."

No comments:

Post a Comment