Feb 7, 2012
TUHUMA ZA UCHAWI ZAHUSISHWA MATUKIO YA MOTO JINJA!!
Familia 18 nchini Uganda zimeachwa bila makazi baada ya matukio kadhaa ya moto kuharibu nyumba zao katika kijiji cha Soweto wilyani Jinja wiki moja iliyopita.
Chanzo cha moto huo bado kinabaki kuwa utata ingawa wakazi wa kijiji hicho wanadai kuwa waganga wa kienyeji wanahusika na matukio hayo.
Mmoja wa wakazi James Wanda,amesema baadhi ya wananchi wa naamini nguvu za giza ndio zimesababisha moto huo kwakuwa kuna waganga wengi wa kienyeji wanaoishi katika kijiji hicho kilichoathiriwa lakini mkuu wa polisi wilayani Jinga Jonathan Musinguzi hakubaliani na tuhuma hizo na kutaka ushirikiano na wananchi kuchunguza suala hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment