HOME

Feb 9, 2012

MJADALA WA KATIBA MPYA..BAADHI YA WABUNGE WATAKA WAKUU WA WILAYA KUTUMIWA KUSIMAMIA UKUSANYAJI MAONI!!


Mjadala mkali umeibuka Bungeni baada ya baadhi ya wabunge kutaka muswada wa marekebisho ya sheria ya  mabadiliko ya katiba kuwatumia wakuu wa wilaya kusimamia shughuli za mchakato wa ukusanyaji maoni ya  katiba.


Wakizungumza wakati wa kutoa maoni ya muswada wa marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba, baadhi ya wabunge wamepinga kifungu 17z(a) cha muswada huo kinachotaka wakurugenzi wa halmashauri kusimamia mchakato huo na kusisitiza kipengele hicho kionyeshe wakuu wa wilaya.


Awali wakiwasilisha maoni ya kamati ya makamu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya katiba sheria na utawala mh. Angellah Kairuki pamoja na msemaji kambi ya upinzani Mheshimiwa Tundu Lissu wamepongeza maamuzi ya serikali kwa kuwatumia wakurugenzi wa halmashauri na kusisitiza yanalenga kufanya mchakato wa ukusanyaji maoni kusimamiwa na watendaji wa serikali.


Mwanasheria mkuu wa serikali, jaji mstaafu Fredrick Werema amesema serikali inapendekeza kuwatumia wakurugenzi wa halmashauri za serikali za mitaa ili kuiwezesha tume kufanyakazi na watendaji hao ya kupokea programu zitakazoendeshwa katika maeneo yao.

No comments:

Post a Comment