HOME

Feb 23, 2012

WATU 50 WAMEKUFA KATIKA SHAMBULIZI IRAQ!!


Takribani watu 50 wamekufa na wengine mamia kujeruhiwa katika mashambulizi ya mabomu na risasi mjini Baghdad.


Maafisa wamesema kuwa mashambulizi hayo yanaonekana kuwalenga zaidi maafisa wa polisi ambapo watu tisa wameuwawa katika shambulizo baya zaidi katikati ya wilaya ya  Karrada ambapo wanaishi watu wa dhehebu la Shia.


Mlipuko karibu na kituo cha polisi umetingisha majengo na kuharibu maduka ambapo hakuna kundi lililojitokeza kudai kuhusika na mashambulizi hayo,Mashambulizi nchini Iraq yameibuka tangu kuondolewa kwa majeshi ya Marekani mwezi Desemba.

No comments:

Post a Comment