HOME

Feb 7, 2012

CHADEMA NA NCCR KUFUTA SHAURI LA KUPINGA UBUNGE WA JIMBO LA KAWE


Vyama vya upinzani vya Chadema na NCCR Mageuzi vya nchini Tanzania vimetangaza kufuta shauri la kupinga ubunge wa jimbo la Kawe, lililofunguliwa katika mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam na mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, Bw. James Mbatia dhidi ya mbunge wa jimbo la Kawe Bi. Halima Mdee.


Katika shauri hilo, aliyekuwa mlalamikaji Bw. James Mbatia alikuwa anaitaka mahakama kuu itengue ushindi wa Mdee kwa madai kuwa alitumia kampeni chafu iliyoambatana na maneno ya kashfa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, hatua aliyodai ilisababisha akose nafasi ya kushinda ubunge wa jimbo la Kawe. 


Akizungumza katika mkutano wa pamoja ulioitishwa na viongozi waandamizi wa vyama hivyo, Katibu mkuu wa Chadema, Dkt. Wilbrod Slaa amesema hatua ya kufuta shauri hilo imezingatia maslahi ya Watanzania hususani wakazi wa jimbo la Kawe ambao kwa muda mrefu wamekuwa na kiu ya kutaka kuona vyama vya upinzani vikungana na kuwa na nguvu ya pamoja.


Kwa mujibu wa Dk. Slaa, makubaliano hayo yanafungua sura mpya ya ushirikiano wa muda mrefu wa kisiasa baina ya vyama hivyo, uhusiano ambao hivi karibuni ulivurugika

No comments:

Post a Comment