HOME

Feb 5, 2012

MCT YAAPISHA MAJAJI WA SHINDANO LA WANAHABARI





Jopo la majaji wanne kati ya tisa katika tuzo ya uandishi wa habari Tanzania (EJAT) mwaka 2011 limeapishwa jana jijini Dar es salaam.


Hii ni mara ya kwanza kwa majaji EJAT kuwaapisha kabla ya kuanza kazi ya kuchambua kazi za wanahabari wa magazeti,radio na televisheni tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo mwaka 2009.


Katika hafla hiyo jopo la majaji hao lilikula kiapo mbele ya jaji mstaafu wa mahakama kuu nchini Thomas Mihayo ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya maadili ya baraza la habari Tanzania (MCT).


Waliokula kiapo ni mwenyekiti wa jopo la majaji Wenceslaus Mushi ambaye ni mhariri msanifu mkuu wa gazet la kampuni ya The Guardian,Attilio Tagalile ,Edda Sanga,Yussuph Omar Chunda,Pili Mtambalike,Prudensia Temba,Mwanzo Millinga na Anaclet Rwegayura.(picha na MCT)

No comments:

Post a Comment