HOME

Feb 3, 2012

TAARIFA YA SERIKALI BUNGENI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI!!


Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii nchini Tanzania Dk. Haji Mponda ameliambia bunge kuwa serikali inatambua kuwa madaktari waliochini ya kamati ya mpito hawapo tayari kufanya mazungumzo na serikali.


Akitoa kauli ya serikali leo bungeni mjini Dodoma Dk. Mponda amesema serikali pia inatambua kuwa mgomo huo wa madaktari si halali kwa kuwa haukuzingatia sheria na taratibu.


Hata hivyo baada ya Waziri Mponda kuwasilisha taarifa hiyo Naibu Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai amependekeza suala la mgomo wa madaktari kupelekwa katika Kamati ya Maadili ya Bunge ili kufanyiwa kazi kwa kina.


Amesema kamati hiyo iliyo chini ya mwenyekiti wake Mhe. Magreth Sitta ikae meza moja na Jumuiya za madaktari,madaktari bingwa pamoja na serikali ili kuweza kujua chanzo na kutafuta suluhu ya suala hilo.

No comments:

Post a Comment