Feb 28, 2012
SHAMBULIO LINGINE NIGERIA!!
Watu wenye silaha wamepanga mashambulzi na kulipua kituo cha polisi na benki iliyokuwa karibu Kaskazini mwa mji Nigeria katika mfulululizo wa mashambulizi mengine ya mabomu yanayodaiwa kufanywa na kundi la waislamu la Boko Haram kwa mujibu wa mashuhuda.
Shambulio hilo katika mji wa Jama'are kaskazini mwa jimbo la Bauchi limetokea saa 24 kabla ya kutokea tukio lingine la ukatili kama hilo katika mji mwingine kaskazini mwa Nigeria ambalo lilisababisha vifo vya askari polisi watatu.
Wakazi wamesema idadi kubwa ya watu wenye silaha walihusika na shambulio siku ya Jumatatu lakini hawakutaja idadi ya majeruhi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment