Feb 9, 2012
MADAKTARI WAKUBALI KUMALIZA MGOMO..KUREJEA KAZINI KESHO!!
Madaktari waliokuwa katika mgomo wamekubali kumaliza mgomo wao na kurejea kazini kesho na kuipa serikali muda wa mwezi mmoja kumaliza madai yao.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya madaktari Dk. Ulimboka Stephen amesema wameamua kuchukua hatua hiyo ya kurudi kazini katika kikao walichokifanya baada ya kukutana na waziri mkuu Pinda leo jijini Dar es salaam ambapo amesema kuanzia kesho madaktari wote nchi nzima watarejea kazini.
Wakati huo Dk. Ulimboka amelitaka jeshi la polisi kuwaachia mara moja watetezi wa haki za binadamu waliokamatwa leo nje ya hospitali ya taifa Muhimbili wakati mazungumzo kati ya madaktari yakiendelea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment