HOME

Feb 9, 2012

MAJOKOFU YA KUHIFADHIA MAITI YASHINDWA KUFANYA KAZI NA KUSABABISHA HALI MBAYA ''MORTUARY''!!


Majokofu katika chumba cha kuhifadhia maiti jijini Nairobi yamekuwa hayafanyi kazi kwa zaidi ya wiki moja sasa, na kusababisha chumba hicho kufanana na sinema ya kutisha.


Miili iliyooza ambayo imepangana katika chumba hicho, baadhi yake ikiwa haijachukuliwa na wahusika, imesababisha kuzaliana kwa wadudu, panya na minyoo, na kusababisha hali ya kusikitisha kwa wafanyakazi na ndugu wa marehemu.


Baadhi ya wafanyakazi wa sehemu hiyo wameamua kuua hisia zao za harufu kwa kunywa pombe kila wakati.


Wakati huo huo, ndugu wa marehemu wanaofika kuchukua miili ya ndugu zao wamekuwa wakipoteza fahamu wanapoona hali za maiti za wapendwa wao.

No comments:

Post a Comment