HOME

Feb 5, 2012

IRAN KUACHA KUUZA MAFUTA ULAYA!!


Waziri wa mafuta wa Iran amekariri kuwa nchi yake itaacha kusafirisha mafuta kwa baadhi ya mataifa ya Ulaya, hata kabla ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya mafuta ya Iran kuanza kutekelezwa mwezi wa July mwaka huu.


Waziri Rostam Qasemi hakueleza nchi gani zitaathirika lakini amesema kutakuwa na mtafaruku katika masoko ya mafuta ya kimataifa, ikiwa mafuta ya Iran yatasusiwa.


Hivi karibuni Umoja wa Ulaya na Marekani, ziliweka vikwazo vipya vikali dhidi ya Iran, wakiishutumu kuwa inatengeneza silaha za nyuklia kisirisiri.

No comments:

Post a Comment