HOME

Feb 9, 2012

WABUNGE WAMETAKIWA KUTOWATETEA WANAFUNZI WANAOFANYA UDANGANYIFU!!


Serikali imewataka wabunge kuacha kuwatetea wanafunzi wanaopewa adhabu kutokana na kubainika
kufanya udanganyifu katika mitihani ya sekondari na shule msingi.


Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi, mheshimiwa  Philipo Mulugo ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la nyongeza  la mbunge wa viti maalum mheshimiwa Suzan Lyimo aliyetakakujua serikali inachukua hatua gani kwa wanafunzi na walimu watakaobainika kufanya udanganyifu.


Amesema serikali itaendelea kutilia mkazo kwa wanafunzi wote watakaofutiwa matokea watapaswa kurudia mtihani baada ya miaka mitatu kama ilivyoanishwa katika sheria ili kukomesha tatizo la udanganyifu katika mitihani lisiendelee kujirudia.

No comments:

Post a Comment