HOME

Feb 8, 2012

SHULE ZA KATA ZAENDELEA KUFANYA VIBAYA MATOKEO KIDATO CHA NNE!!

Baraza la mitihani nchini Tanzania leo limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne kwa wanafunzi waliofanya mtihani huo mwaka jana huku kukiwa na ongezeko la kiwango cha ufaulu ikilinganishwa na matokeo yaliyotolewa mwaka jana.

Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam leo, katibu mkuu wa baraza hilo, Dk. Joyce Ndalichako amesema shule binafsi zimeoongoza kwa ufaulu huku shule za kata zikiendelea kufanya vibaya.

Kwa mujibu wa Dkt Ndalichako, ongezeko la ufaulu limeenda sambamba na kiwango cha udanganyifu ambapo jumla ya wanafunzi elfu tatu mia tatu na tatu wamefutiwa matokeo yao baada ya kubainika kufanya udanganyifu.

No comments:

Post a Comment