Feb 24, 2012
NIPO NA NITAENDELEA KUWEPO THT - AMINI!!
Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Jumba la vipaji Tanzania (THT), Amini Mwinyimkuu almaarufu kama Amini amekanusha uvumi uliopo mtaani na kuripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini kuwa amefukuzwa katika Jumba hilo la vipaji (THT).
Akizungumza na Blog hii Amini ambaye ni mpenzi zilipendwa wa mwanamuziki Linah amesema ameshangazwa sana na uvumi huo wa kuwa yeye(Amini) amefukuzwa THT na kuongeza kuwa habari hizo hazina ukweli na ni uzushi mtupu.
Hata hivyo amesema anafikiri kuwa uzushi huo umetokana na ukimya wake wa kutotoa wimbo wowote kwa kipindi kirefu na kuongeza kuwa tayari amesharekodi wimbo wake mpya alioupa jina la ni wewe ambao anatarajia kuanza kuusambaza kwenye vituo mbalimbali vya Redio mapema wiki ijayo.
ZAIDI:ZAMA HUMU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment