HOME

Feb 9, 2012

UGANDA KUANZA KUTENGENEZA ARV!!


Kampuni ya dawa nchini Uganda ya Quality Chemicals, kuanzia mwezi ujao itaanza kutengeza dawa za kurefusha maisha (ARV) aina ya Tenofovir.


Matumizi ya mwezi mmoja ya dawa hiyo itagharimu shillingi za Uganda elfu 44,000 ukilinganisha na dawa zinaziofafanana na hizo
zinazoagizwa kutoka nje ambazo zinauzwa kwa shillingi millioni moja laki nne za Uganda.


Mfamasia wa kampuni hiyo Samuel Opio amesema kidonge kimoja kinatumika kwa siku badala ya vidonge viwili ambavyo vinatolewa
na tiba kutoka nje.

No comments:

Post a Comment