Bw. James Ibori |
Aliyekua Gavana wa mojawapo wa majimbo yanayozalisha mafuta kwa wingi nchini Nigeria James Ibori, amekiri katika mahakama ya Uingereza ,mashataka kumi ya kuhusika na biashara haramu ya fedha na pia njama ya kughushi.
Polisi wa Uingereza wanamshtumu kwa kuiba takriban dolla $400m katika kipindi cha miaka 8.
Bw Ibori, ambae wakati mmoja alichukuliwa kua mmojawapo wa wanasiasa tajiri na mwenye ushawishi mkubwa alikamatwa mnamo mwaka 2007.
Baadae aliachiliwa ,kabla ya kukamatwa tena mjini Dubai kutokana na hati ya Uingereza na kusafirishwa hadi Uingereza.
Mnamo mwaka 2007, mahakama ya Uingereza ilipiga tanji mali zake zote zilizoshukiwa kuwa za thamani ya dolla millioni 35.
Mshahara wake kama gavana wa jimbo la Delta ulikua chini ya dola 25,000.
No comments:
Post a Comment