HOME

Feb 21, 2012

AHAKAMA KUU YAKUBALI TANESCO KUIPINGA DOWANS!!


Mahakama Kuu Dar es Salaam imerejesha matumaini kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) baada ya kutupilia mbali pingamizi la Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans dhidi ya maombi yake ya kibali cha kukata rufaa.


Tanesco iliwasilisha maombi mahakamani hapo kutaka kibali cha kukata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga hukumu ya mahakama hiyo iliyoamuru kusajiliwa kwa tuzo ya Dowans ya Sh94 bilioni, iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC).


Hata hivyo, Dowans nayo kupitia kwa wakili wake, Kennedy Fungamtama iliweka pingamizi dhidi ya Tanesco ikiiomba mahakama hiyo iinyime kibali hicho cha kukata rufaa kwa madai kuwa haina haki ya kisheria kupinga hukumu hiyo.


ZAIDI:INGIA HUMU

No comments:

Post a Comment