HOME

Feb 16, 2012

MAUAJI YAKITHIRI LIBYA!!


Shirika la kutetea haki za binadamu, Amnesty International linasema visa vya mateso, mauaji na watu kuzuiliwa bila kufunguliwa mashataka vimekithiri nchini Libya.


Shirika hilo linasema ukiukaji huo unatekelezwa na makundi ya wapiganji waliojihami ambao walimng'oa Muammar Gaddafi madarakani.


Walioathirika zaidi ni watu wanaohofiwa kuwa wafuasi wa Gaddafi, waafrika weusi na wahamiaji walioko Libya.


Kufuatia visa hivyo makundi ya watu waliolengwa sana na visa hivyo wamehama makaazi yao.


Shirika la Amnesty international linasema serikali mpya ya Libya imeshindwa kuwachukulia hatua watu wanaotekeleza vitendo hivyo.

No comments:

Post a Comment