HOME

Feb 17, 2012

KAMATI YA BUNGE YAIBUA UFISADI WIZARA YA MALIASILI!!


Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kuu (PAC) imebaini utata wa matumizi ya zaidi ya Sh25 bilioni katika Wizara ya Maliasili na Utalii, huku watendaji wa wizara hiyo wakikosa takwimu za idadi ya wanyamapori na vitalu vya uwindaji.


Kashfa hiyo imezidi kuitikisa wizara hiyo kwani hivi karibuni ilikumbwa na kashfa nyingine ya utoroshaji nje twiga wakiwa hai, kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).


Jana, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa PAC, John Cheyo alisema fedha hizo zinatokana na mapato kutoka vyanzo mbalimbali vya wizara hiyo.

No comments:

Post a Comment