Seven Mosha, mwakilishi wa Sony Music and Rockstar4000 Tanzania |
Kwa mara ya kwanza Tanzania, msanii wa Gospel, Rose Muhando amepata shavu kubwa ikiwa ni dili ya kurekodi miziki na kampuni heavyweight duniani ya muziki ya Sony.
Msemaji wa Kampuni ya Sony music Africa Maunsha Sarawan amesema kwamba Rose, kwa muda wa miaka mitano, atarekodi album ya nyimbo mpya kabisa, shughuli itakayofanywa nje ya nchi, pamoja na kufanya tour ya muziki kupromote nyimbo zake na vilevile kufanyiwa rebranding kumpa mwanamuziki huyo muonekano tofauti wa kipekee.
Akiongelea mkataba huo, Rose alimshukuru Mungu kwa kumpa nafasi hiyo ya kipekee, na kuwashukuru waliomuwezesha kimuziki miaka mingi ya yeye kuwepo kwenye industry.
Wasanii ambao wako chini ya usimamizi wa kampuni ya Rockstar4000 ambao waliwahi kufanya project ya Airtelone8 wakimishirikisha Alikiba walikuwepo akiwemo AliK mwenyewe, AY, MwanaFA, na Diamond Platinum walijitokeza kuonyesha support.
Thanks: http://www.bongo5.com
No comments:
Post a Comment