HOME

Feb 3, 2012

MAHAKAMA NCHINI KENYA IMEPIGA MARUFUKU MAJADILIANO HADHARANI YA RUTO NA KENYATTA.


Mahakama kuu nchini Kenya imetoa amri ya kupiga marufuku majadiliano hadharani ya wagombea wa nafasi ya urais naibu waziri mkuu Uhuru Kenyatta na William Ruto katika uchaguzi mkuu ujao mpaka hapo mahakama hiyo itakapoamua juu ya suala hilo.


Jaji Isaac Lenaola ametoa amri hiyo jana kufuatia ombi lililowasilishwa na wapiga kura watatu na vyama vya kiraia viwili ambavyo vinataka kuzuiwa kwa Kenyatta na Ruto kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao.


Hoja iliyowasilishwa katika mahakama ya katiba inadai kuwa Kenyatta na Ruto hawatakiwi kushika ofisi ya umma baada ya majaji wa mahakama ya kimataifa ya makosa ya uhalifu ICC waliosikiliza shauri la awali la kudhibitisha mashitaka dhidi ya watumuhimiwa hao kuwaona kuwa wana kesi ya kujibu.

No comments:

Post a Comment