WATOVU WA NIDHAMU WAREJESHWA SHULENI!!
Shule ya Sekondari Madangwa imewarejesha masomoni wanafunzi 19 waliokuwa wametimuliwa mwaka mmoja uliopita kwa kukosa nidhamu.
Kati ya wanafunzi waliorejeshwa; wavulana ni 16 na wasichana watatu wa kidato cha pili, watatu wa kidato cha nne waliokuwa wametimuliwa shuleni hapo Mei 19 mwaka wa jana.
Mkuu wa shule hiyo Nelsoni Lupogo amesema kuwa wanafunzi hao wamerejeshwa mwanzoni mwa mwezi uliopita, baada ya uongozi wa shule hiyo kupokea barua ya kuomba msamaha kutoka kwa wanafunzi husika.
No comments:
Post a Comment