HOME

Feb 9, 2012

TANESCO LATOLEA UFAFANUZI SUALA LA KUKATIKA KWA UMEME JANA NA LEO!!

Meneja mawasiliano wa TANESCO, Bi Badra Masoud

Shirika la umeme nchini Tanzania TANESCO limetoa ufafanuzi kuhusiana na matukio ya kukatika umeme yaliyolikumba jiji la Dar es Salaam kwa siku za jana na leo.


Meneja mawasiliano wa TANESCO, Bi Badra Masoud amesema kukatika kwa umeme kumetokana na hitilafu katika vituo vya kusambazia umeme vya ununio Kunduchi, Kijitonyama pamoja na kituo cha Masaki.


Kwa mujibu wa Bi. Masoud, mafundi wa umeme wanaendelea na zoezi la kuhakikisha huduma hiyo inarejea kama kawaida.

No comments:

Post a Comment