Waziri wa mawasiliano,sayansi na teknolojia, Prof. Makame Mbarawa |
Vyombo vyote vya habari vinavyorusha matangazo yake kwa mfumo wa tekonolojia ya analojia nchini Tanzania, vimeagizwa kuwa ifikapo Disemba thelathini na moja mwaka huu, viwe vimezima mitambo yao na kuanza kurusha matangazo kwa kutumia mfumo wa teknolojia ya digitali.
Waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa ametoa agizo hilo ambalo ni sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa na nchi za Afrika Mashariki wa kuhakikisha ifikapo mwaka 2013 matangazo yote ya radio na televisheni yawe yanapatyikana kwa mfumo wa teknolojia ya digitali.
Kwa mujibu wa Prof. Mnyaa, serikali inatambua athari yas gharama zitakazowakumba watumiaji wa huduma za matangazo ya radio na televisheni ambao watatakiwa kununua ving'amuzi na kwamba inafikiria uwezekano wa kuwataka waagizaji wa vifaa vya digitali kupunguza bei ya vifaa hivyo ili watu w asio na uwezo wamudu kuvinunua.
No comments:
Post a Comment