Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda |
Kasi ya mauaji ya kutisha yanayotokea katika mji wa Songea mkoani Ruvuma inazidi kuongezeka kufuatia mtu mmoja kuuawa usiku wa kuamkia leo mwaka huu katika eneo la Lizaboni mjini Songea ambapo mwili wake ulikutwa ukiwa umekatwa katwa kwa kutumia mapanga.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa awali waliokuta mwili wa marehu huyo aliyejulikana kwa jina la Bakari Ally(20) mkazi wa Lizaboni walisema kuwa alikuwa na muda wa miezi minne tangu afike hapo akitokea Tunduru na kupata kazi katika mashine ya kusaga nafaka ambayo alikuwa akiifanya mpaka mauti hayo yalipomkuta.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Februari 20 mwaka huu ambapo uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa marehemu aliuawa kwa kukatwa katwa na mapanga sehemu mbali mbali za mwili wake ikiwemo kichwani.
No comments:
Post a Comment