Chama cha walimu nchini Tanzania (CWT) kimeitaka serikali kuanzia mwaka ujao wa fedha, kuongeza kiwango cha mishahara ya walimu kwa asilimia mia moja ili kukidhi kupanda kwa gharama za maisha.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, naibu katibu mkuu wa CWT Bw. Ezekiah Oluoch amesema madai ya nyongeza hiyo yanatokana na kupanda kwa gharama za maisha kunakowafanya walimu waishi katika mazingira magumu.
Aidha, Bw. Oluoch ameitaka serikali kuketi katika meza ya mazungumzo na chama hicho kabla ya Aprili mwaka huu, ili makubaliano yatakayofikiwa yawakilishwe katika bunge lijalo la bajeti ili nyongeza hiyo ianze kutolewa katika mwaka ujao wa fedha.
No comments:
Post a Comment