HOME

Feb 28, 2012

MCHUANO MKALI UCHAGUZI SENEGAL!!

Rais Abdoulaye Wade akipiga kura yake

Mchuano mkali unaendelea katika uchaguzi wa Urais wenye utata nchini Snegal kati ya Rais wa sasa Abdoulaye Wade na waziri mkuu wa zamani Macky Sall.


Taarifa za awali kutoka Senegal ambazo hazijathibitishwa zinaonyesha kuwa kuna mchuano mkali kati ya Rais wa sasa Abdoulaye Wade na waziri mkuu wa zamani Macky Sall na vyombo vya habari vya ndani na Bw Sall vinasema hakuna mgombea aliyefikia 50% inayotakiwa kuepuka duru ya pili.


Rais Wade, 85, anawania kwa awamu ya tatu nafasi hiyo licha ya kutumikia vipindi viwili vinavyoruhusiwa na katiba.


Bw. Wade alizomewa wakati alipokwenda kupiga kura Jumapili katika mji mkuu,Dakar.

No comments:

Post a Comment