HOME

Feb 21, 2012

HAYE,CHISORA KUKABILIWA NA KIFUNGO!!

David Haye

Mabondia wa Uingereza David Haye na Dereck Chisora wanatuhumiwa kutenda makosa ya uhalifu ambayo adhabu yake ni kifungo baada kupigana hadharani huko Munich.


Waendesha mashtaka wa Ugerumani wameliambia shirika la utangazaji la Uingereza BBC kuwa bondia Haye anatuhumiwa kusababisha maumivu ya mwili ambalo ni kosa la jinai na ikiwa atatiwa hatiani adhabu yake ni miezi sita mpaka miaka kumi jela.


Chisora ambaye amekubali kuwa kitendo alichofanya hakikubaliki anatuhumiwa kujeruhi ikiwa ni pamoja na kutoa lugha ya vitisho kosa hilo adhabu yake ni miaka mitano jela.

No comments:

Post a Comment