HOME

Feb 3, 2012

NJAA IMEKWISHA SOMALIA!!


Umoja wa mataifa umetangaza kuwa baa la njaa nchini lililotangazwa kukumba taifa la Somalia sasa limefikia kikomo.


Umoja huo umesema hali imeimarika nchini humo kutokana na mavuno mazuri na misaada ya kibinadamu inayoendelea kutolewa.


Mwezi uliopita mshirikishi mkuu wa shughuli za umoja uhuo nchini Somalia Mark Bowden alisema maelfu ya watu wamekufa tangu mwezi julai mwaka uliopita kutokana na baa la njaa.


Afisa mkuu wa shirika la umoja wa mataifa kuhusu chakula na kilimo FAO Jose Granziano amesema mvua kubwa iliyonyesha pamoja na misaada ya kibinadam iliyotolewa imechangia pakubwa kuimarika kwa hali ya maisha nchini somalia.

No comments:

Post a Comment