HOME

Feb 12, 2012

BREAKING NEWS...MWANAMUZIKI MASHUHURI WHITNEY HOUSTON AFARIKI DUNIA!!

R.I.P. Whitney Houston - (August 9, 1963—February 11, 2012)

Mwanamuziki mashuhuri kutoka nchini Marekani Whitney Houston amefariki dunia jana akiwa na umri wa miaka 48.


Kwa mujibu wa mwandishi wake wa habari Kristen Foster,Sababu za kifo chake na mahala alipofariki bado hazifahamiki ingawa kuna taarifa zinadai Witney amekufa akiwa katika chumba cha hoteli.


Akiwa mmoja wa wanamuziki wenye mafanikio makubwa duniani, pia aliwahi kuwa mcheza filamu, katika michezo kama vile The Bodyguard na Waiting to Exhale.


Witney ameweka rekodi ya kushinda tuzo 415 ambapo 2 ni za Emmy,6 za Grammy,22 za American Music na 30 za chati za muziki Billboard.

No comments:

Post a Comment