HOME

Feb 24, 2012

MWIGIZAJI DOTNATA AFANYIWA UPASUAJI!!

Husna Posh

Mtayarishaji na mwigizaji wa filamu Swahiliwood Husna Posh ‘Dotnata’ wiki iliyopita alifanyiwa upasuaji mkubwa kutokana na matatizo ya tumbo baada ya kuugua ghafla na kulazwa katika Hospitali ya THI iliyopo Kinondoni akiongea na FC nyumbani kwake Dotnata amesema kuwa anamshukru Mungu kwa kufanyiwa upasuaji mkubwa na kuamka salama na kuweza kuendelea na hali yake vema kwani tatizo lilikuwa kubwa.


“Namshukru kwanza Mungu wangu pili ni hawa Madaktari waliofanikisha zoezi hili na kunirudisha katika hali yangu ya kawaida, sasa naendelea vema kwa sasa muda mwingi nitatumia kwa mapumziko huku nikiendelea na matumizi ya dawa, lakini kwa sasa nipo safi kabisa na madaktari wangu ni mabingwa na walitoka nje kwa ajili ya kazi hiyo tu,”alisema Dotnata.
Husna Poshi


Kutokana na upasuaji huo Dotnata amesema kuwa anatakiwa kupumzika kwa muda wa miezi sita bila kufanya kazi yoyote nzito wala haruhusiwi kuendesha gari, kwa mantiki hiyo hata kuigiza atahitaji kuigiza zile sehemu zisozo na kurupushani kwa kufanya hivyo anaweza kupata matatizo. 

Chanzo:FilamuCentral

No comments:

Post a Comment