HOME

Feb 23, 2012

WAYNE ROONEY KUIKOSA MECHI DHIDI YA AJAX!!

Mshambuliaji Wayne Rooney

Mshambuliaji Wayne Rooney atakosa mchezo wa leo wa marudiano wa ligi ya Europa dhidi ya Ajax kutokana na kukabiliwa na maambukizi kwenye koo lake.


Rooney alikuwepo kwenye mazoezi hapo jana akiwa na wachezaji wenzake wa Manchester United, lakini alirejeshwa nyumbani kutokana na kuwa mgonjwa.


Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson, amesema anampumzisha mchezaji huyo, akiwa na matumaini ifikapo jumapili atakuwa fiti kwa mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Norwich.

No comments:

Post a Comment