Feb 8, 2012
MADAKTARI HOSPITALI YA BUGANDO WAJIUNGA RASMI KWENYE MGOMO!!
Huduma za afya katika hospitali ya rufaa ya Bugando iliyopo jijini Mwanza zimeanza
kuzorota baada ya madkatari ambao siyo mabingwa kuanza rasmi kugoma kuungana na wenzao wa hospitali ya taifa ya Muhimbili, KCMC na hospitali ya rufaa ya Mbeya kudai maslahi yao.
Mgomo huo umeanza baada ya madkatari wanafunzi, madaktari wa kawaida na wale wanaosomea udaktari bingwa wapatao 150 kukutana jana na kuazimia kuunga mkono wenzao kwa kusitisha huduma zote hata zile za dharura.
Baadhi ya wagonjwa waliokaa tangu asubuhi hospitalini hapo mpaka alasiri bila kupata huduma huku wengine hasa wa upande wa kliniki ikiwemo ya upasuaji na kisukari wakiandikiwa na manesi tarehe nyingine za kurudi ingawa walikuwa wameishalipia shilingi 3,000 za kumwona daktari.
Katika hali ya kushangaza, Kaimu mkurugenzi wa hospitali hiyo Dk. Japhet Giliyoma amekataa kuzungumzia sakata hilo na kuzuia waandishi kuingia wodini kuhoji wagonjwa kwa madai kuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza amekataa na ndiye atakayetoa tamko juu ya mgomo huo hapo kesho
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment