HOME

Feb 9, 2012

SERIKALI YAWASIMAMISHA KAZI MAAFISA WA NGAZI YA JUU WIZARA YA AFYA!!

Waziri mkuu Mizengo Pinda akisikiliza kwa makini madaktari kwa makini leo jijini Dar es salaam.


Madaktari wakimsikiliza Mhe. Pinda.

Waziri mkuu nchini Tanzania, Mizengo Pinda, leo ametangaza kuwasimamisha kazi katibu mkuu wizara ya afya, Bi Blandina Nyoni na mganga mkuu wa serikali, Dkt Deo Mtasiwa.


Akizungumza na jopo la madaktari walio katika mgomo, mheshimiwa Pinda amesema serikali imechukua uamuzi huo ili kupisha tuhuma zinazowakabili viongozi hao kuwa wamehusika na uzembe uliosababisha kutokea kwa mgomo.


Aidha, mheshimiwa Pinda amesema serikali imekubali kuongeza kiwango cha posho ya kuitwa kazini kw madaktari hao sambamba na kuunda tume itakayoishauri kuhusiana na madai nane ya madaktari hao ikiwemo nyongeza ya mshahara ya shilingi milioni tatu na laki tano kama kima cha chini

No comments:

Post a Comment